naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 10

Vijana wakitumia maarifa wanayopata katika taasisi za kielimu wanaweza kuunda bidhaa humu humu nchini ili tuache kutegemea za kwingine. Fupisha ujumbe huu kwa…

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kuandika, Ufupisho

UFUPISHO.
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 9 hadi la 12.

Nchi yetu imetunukiwa maliasili ya aina mbalimbali. Kati ya rasilimali hizo ni maanguko ya maji, mito, bahari, maziwa, milima, mabonde na wanyama kama vile ndovu, nyati, fisi, simba, duma na wengine wengi. Tunapaswa kuyatunza maliasili haya na kuyatumia kwa uwajibikaji ili taifa letu liweze kuimarika kiuchumi.

Inasikitisha kuona kwamba bado tunaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kutokana na ukosefu wa viwanda. Vijana wakitumia maarifa wanayopata katika taasisi za kielimu wanaweza kuunda bidhaa humu humu nchini ili tuache kutegemea za kwingine. Manufaa ya elimu ni chungu nzima.

Mwito wangu ni kuwa tufikirie namna tunavyoweza kujiendeleza kwa rasilimali zetu wenyewe. Tukiendelea na tabia yetu ya kukopa na kuomba misaada kutoka kwingine tutaishi kuwa hohehahe bila ya kuwa na mbele wala nyuma. Tunaweza kuondoa uhitaji wetu kabisa tukiutambua umuhimu wa rasilimali zetu tulizo nazo na kuzitumia kwa njia yenye manufaa.

10) Vijana wakitumia maarifa wanayopata katika taasisi za kielimu wanaweza kuunda bidhaa humu humu nchini ili tuache kutegemea za kwingine.
Fupisha ujumbe huu kwa maneno yasiyozidi kumi.

Answer

Vijana watumie elimu yao kuunda bidhaa ili tuache utegemezi.

Ufupisho unabaki na wazo kuu (vijana kutumia elimu kuunda bidhaa nchini ili tusitegemee nchi nyingine) kwa maneno machache: hapa ni maneno tisa.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test