naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 9

Andika habari kuu katika aya ya kwanza kwa sentensi moja.

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kuandika, Ufupisho

UFUPISHO.
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 9 hadi la 12.

Nchi yetu imetunukiwa maliasili ya aina mbalimbali. Kati ya rasilimali hizo ni maanguko ya maji, mito, bahari, maziwa, milima, mabonde na wanyama kama vile ndovu, nyati, fisi, simba, duma na wengine wengi. Tunapaswa kuyatunza maliasili haya na kuyatumia kwa uwajibikaji ili taifa letu liweze kuimarika kiuchumi.

Inasikitisha kuona kwamba bado tunaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kutokana na ukosefu wa viwanda. Vijana wakitumia maarifa wanayopata katika taasisi za kielimu wanaweza kuunda bidhaa humu humu nchini ili tuache kutegemea za kwingine. Manufaa ya elimu ni chungu nzima.

Mwito wangu ni kuwa tufikirie namna tunavyoweza kujiendeleza kwa rasilimali zetu wenyewe. Tukiendelea na tabia yetu ya kukopa na kuomba misaada kutoka kwingine tutaishi kuwa hohehahe bila ya kuwa na mbele wala nyuma. Tunaweza kuondoa uhitaji wetu kabisa tukiutambua umuhimu wa rasilimali zetu tulizo nazo na kuzitumia kwa njia yenye manufaa.

9) Andika habari kuu katika aya ya kwanza kwa sentensi moja.

Answer

Tunapaswa kuyatunza maliasili yetu na kuyatumia kwa uwajibikaji ili taifa letu liimarike kiuchumi.

Aya ya kwanza inataja maliasili ya nchi, kisha inasisitiza kuyatunza na kuyatumia kwa uwajibikaji ili taifa liimarike kiuchumi.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test