naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 8

Neno sepetu lina maana sawa na beleshi. Kisawe cha neno dhati ni?

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 5 hadi la 8.

Ingawa serikali za magatuzi mbalimbali zina jukumu kubwa katika kudumisha usafi katika maeneo ya miji, wakazi wa maeneo hayo hawafai kujipakatia mikono huku wakingojea kufanyiwa kila kitu. Lazima wawajibike ipasavyo kwa kuchukua hatua ambazo hazitavuruga mazingira na kuishia kuwa kero na hatari kwao na wenzao.

Mathalani, wakaazi wanaweza kutenga siku katika mwezi ambapo watashiriki kwa pamoja shughuli za kudumisha usafi ikifika siku hiyo, wajitokeze kwa wingi huku wamebeba sepetu, reki, kwanja na vifaa vingine muhimu. Ni muhimu wavalie mavazi yafaayo ili kujikinga dhidi ya athari zitokanazo na uchafu kama vile kudungwa na vitu vyenye kuathiriwa na bakteria katika uchafu.

Usafi wa mazingira ni jambo linalopaswa kuzingatiwa kwa dhati na kila mmoja. Uchafuzi wa mazingira unaofanywa na watu wenye mapuuza unaweza kuwa chanzo cha majuto baadaye.

8) Neno sepetu lina maana sawa na beleshi. Kisawe cha neno dhati ni?

  1. AUangalifu.
  2. BUaminifu.
  3. CLengo.
  4. DBidii.

Answer

B. Uaminifu.

Kufanya jambo kwa dhati ni kulifanya kwa moyo wa kweli, yaani kwa uaminifu.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test