CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 19
Ukosefu wa usalama huathiri vipi elimu ya watoto?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu swali la 14 hadi 20.
Ukosefu wa usalama ni hali ambapo watu hawako huru kuishi bila hofu ya kudhuriwa au kupoteza mali zao. Hali hii inaweza kusababishwa na mambo kama uhalifu, vita, ukosefu wa ajira, matumizi ya dawa za kulevya, au ukosefu wa usalama, watu huishi kwa wasiwasi na mara nyingi hushindwa kufanya shughuli zao za kila siku kwa ufanisi, kama vile biashara au masomo.
Madhara ya ukosefu wa usalama ni makubwa kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Kwanza, husababisha vifo, majeraha na uharibifu wa mali, vilevile hupunguza maendeleo ya kiuchumi kwa sababu wawekezaji hukwepa maeneo yasiyo salama. Pia watoto wanaweza kushindwa kwenda shule na hivyo kuathiri elimu yao. Aidha, ukosefu wa usalama husababisha hofu na msongo wa mawazo miongoni mwa wananchi, jambo linalodhoofisha mshikamano wa kijamii.
19. Ukosefu wa usalama huathiri vipi elimu ya watoto?
- AHuongeza shule.
- BHufanya walimu kuongeza.
- CHuwazuia kuenda shule.
- DHuwafanya kupoteza nia yao ya masomo
Answer
C. Huwazuia kuenda shule.
"Watoto wanaweza kushindwa kwenda shule."
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Wawekezaji hufanya nini katika maeneo yasiyo salama?Question 20
- Je, mazungumzo haya yanafanyika wakati gani?Question 21
- Ni kweli kusema kuwa makake ZawadiQuestion 22
- Neno Mola limetumika katika kifungu hiki, ni lipi si kisawe chake?Question 23
- Ni nani aliyemtuma Zawadi madukani?Question 24
- Babu alimwomba Zawadi afanye nini arudipo kwao?Question 25