naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 18

Neno ajira limetumika katika kifungu hiki, ni sawa kimaana na?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu swali la 14 hadi 20.
Ukosefu wa usalama ni hali ambapo watu hawako huru kuishi bila hofu ya kudhuriwa au kupoteza mali zao. Hali hii inaweza kusababishwa na mambo kama uhalifu, vita, ukosefu wa ajira, matumizi ya dawa za kulevya, au ukosefu wa usalama, watu huishi kwa wasiwasi na mara nyingi hushindwa kufanya shughuli zao za kila siku kwa ufanisi, kama vile biashara au masomo.
Madhara ya ukosefu wa usalama ni makubwa kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Kwanza, husababisha vifo, majeraha na uharibifu wa mali, vilevile hupunguza maendeleo ya kiuchumi kwa sababu wawekezaji hukwepa maeneo yasiyo salama. Pia watoto wanaweza kushindwa kwenda shule na hivyo kuathiri elimu yao. Aidha, ukosefu wa usalama husababisha hofu na msongo wa mawazo miongoni mwa wananchi, jambo linalodhoofisha mshikamano wa kijamii.

18. Neno ajira limetumika katika kifungu hiki, ni sawa kimaana na?

  1. AKazi
  2. BWaajiriwa
  3. CWaajiri
  4. DPesa

Answer

A. Kazi

Ajira ni kazi.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test