CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 24
Ni nani aliyemtuma Zawadi madukani?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali 21 hadi 25.
Babu: Hujambo Zawadi
Zawadi: Sijambo babu, shikamoo?
Babu: Marahaba mjukuu wangu.
Zawadi: Umeamkaje babu?
Babu: Nimeamka salama salmini. Ninashukuru Mola. Je watu ni salama huko nyumbani?
Zawadi: Isipokuwa nina ambaye ana homa, wengine wote wako wazima kama kigongo.
Babu: Na apate afueni ya haraka huyo binti yangu. Waelekea wapi asubuhi hii mjukuu.
Zawadi: Baba amenituma kumtafutia nina dawa ya homa huko madukani.
Babu: Sawa, harakisha usije ukachelewa basi.
Zawadi: Asante babu. Kua na siku njema.
Babu: Nawe pia mjukuu wangu. Wape salamu zangu nyumbani
24. Ni nani aliyemtuma Zawadi madukani?
- AMama yake
- BNdugu yake
- CBabu yake
- DAbu yake
Answer
D. Abu yake
"Baba amenituma": abu ni baba.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Babu alimwomba Zawadi afanye nini arudipo kwao?Question 25
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 26.Question 26
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 27.Question 27
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 28.Question 28
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 29.Question 29
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 30.Question 30