CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 21
Je, mazungumzo haya yanafanyika wakati gani?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali 21 hadi 25.
Babu: Hujambo Zawadi
Zawadi: Sijambo babu, shikamoo?
Babu: Marahaba mjukuu wangu.
Zawadi: Umeamkaje babu?
Babu: Nimeamka salama salmini. Ninashukuru Mola. Je watu ni salama huko nyumbani?
Zawadi: Isipokuwa nina ambaye ana homa, wengine wote wako wazima kama kigongo.
Babu: Na apate afueni ya haraka huyo binti yangu. Waelekea wapi asubuhi hii mjukuu.
Zawadi: Baba amenituma kumtafutia nina dawa ya homa huko madukani.
Babu: Sawa, harakisha usije ukachelewa basi.
Zawadi: Asante babu. Kua na siku njema.
Babu: Nawe pia mjukuu wangu. Wape salamu zangu nyumbani
21. Je, mazungumzo haya yanafanyika wakati gani?
- AMchana
- BJioni
- CAsubuhi
- DAdhuhuri
Answer
C. Asubuhi
"Waelekea wapi asubuhi hii."
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Ni kweli kusema kuwa makake ZawadiQuestion 22
- Neno Mola limetumika katika kifungu hiki, ni lipi si kisawe chake?Question 23
- Ni nani aliyemtuma Zawadi madukani?Question 24
- Babu alimwomba Zawadi afanye nini arudipo kwao?Question 25
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 26.Question 26
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi 27.Question 27