naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 5

Funzo kuu hasa linalotokana na hadithi hii ni lipi? (Alama 2)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 2 marks · Topic: Kusoma, Ufahamu

UFAHAMU WA KUSOMA
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi 4
Urafiki kati ya Simba na Fisi ulishinda ule wa ndugu wa toka nitoke. Mmoja alipopatwa na tatizo, aliyehisi uchungu ni huyo rafikiye. Wanyama walishauriwa kuiga urafiki wa simba na fisi. Wanyama walipendezwa hasa na jinsi marafiki hao walivyochuma pamoja kuzikidhia familia zao mahitaji ya kimsingi.
Hali iliendelea kuwa hivyo hadi wanyama hao walipooa na kuzaa watoto. Ndoa zao zikaleta mabadiliko makubwa katika maisha yao. Vinywa vya kulishwa vikaongezeka. Ikawa vigumu kuandamana pamoja usasini kutokana na ulezi wa watoto. Wakaafikiana kuwinda kwa zamu mmoja akiachwa kuwatunza watoto kwa kuwa wake wao waliaga tu pindi walipojifungua. Hata hivyo kila wakati fisi alipobaki nyumbani, chakula kilipungua kwa kiasi kikubwa ghalani.
Simba alipouliza sababu ya chakula kupungua, fisi angesema, “Gharama ya maisha imepanda, ulezi wa watoto ni changamoto kubwa. Licha ya hayo tuna wezi pia. Chatu amejaribu kuwala watoto wetu mara kadhaa. Nimepambana naye leo nikafanikiwa kuwaokoa. Nilipoingia chumbani kuwafungia huko, alipata nafasi ya kutoweka na kasi fulani cha chakula.”
Hulka hii ya Fisi iliendelea kwa muda mrefu huku Simba akimshuku. Kila chakula kilipotoweka, Fisi angemdanganya “Leo Simba anayefanana na wewe ameiba chakula na kutorokea mtoni.” Jambo hilo lilimkasirisha Simba akakata shauri kumwandama adui huyo aliyewahangaisha. Simba alisimama ukingo wa mto na kuyatazama maji yaliyotulia. Ndani ya maji hayo, alimwona Simba mwenzake waliyefanana.
“Lahaula! Kumbe ni kweli huyu ndiye amekuwa akituibia?” Simba alijiuliza.
Kwa hasira Simba alimrukia mwenzake aliyekuwa majini. Lakini alijipata akipiga kivuli chake majini. Ghafla kaumwa na mamba majini. Wakapigana kwa muda mrefu. Hatimaye wote wakachoka na kila mmoja kujiendea zake. Simba akagundua amekuwa akidanganywa. Alipofika nyumbani alipata Fisi na watoto wake wametoweka.

4. Funzo kuu hasa linalotokana na hadithi hii ni lipi? (Alama 2)

Answer

Tuwe marafiki wa kweli; udanganyifu na ubinafsi huharibu urafiki.

Fisi alimtendea Simba nini?

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test