CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 16
Neno “kukithiri” limetumika katika kifungu hiki. Maana yake ni:
From Kiswahili Paper 1 — October 2026 Collection · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa kusoma
Unyanyasaji wa kijinsia ni jambo lililopitwa na wakati. Kinyume na hali ilivyo sasa, jamii nyingi zimeona mwanga. Baadhi ya wanaojihusisha na vitendo hivi hujikuta mashakani. Uvundo uliozagaa na kukithiri katika jamii kutokana na vitendo hivi hudhihirisha udhalilishaji wa jinsia.
Aghalabu, ni watu wanaojulikana katika jamii ndio wanaojihusisha na vitendo hivi. Ukweli ni kuwa binadamu hawapaswi kudhalilishana. Visa vya ubakaji havitokani na sababu moja tu, bali hutokana na unyama ulio ndani ya mbakaji. Hiki ni kitendo cha aibu, na athari zake ni mbaya sana kwa wahanga. Baadhi hupata magonjwa ya zinaa na wengine hupoteza maisha mikononi mwa wahalifu.
Jambo la kusikitisha ni kuwa vitendo hivi vya kinyama hutekelezwa na watu wanaojulikana katika jamii. Vyaweza kutokea nyumbani, kazini, njiani na hata mitaani. Shime jamani! Tuungane sote ili tuweze kukomesha unyanyasaji wa aina yoyote wa kijinsia. Vijana, wazee, wazazi na jamii kwa jumla, ni jukumu letu kukabili maovu haya. Tuache utashi wa moyo na tuwasaidie wenzetu wanaokabiliwa na vitendo hivi viovu.

- AKuongezeka
- BKupungua
- CKukemewa
- DKuendelezwa
Answer
A. Kuongezeka
Kukithiri ni kuongezeka au kuzidi kiasi.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Maana ya nahau “utashi wa moyo” ni:Question 17
- Ni kijana yupi aliyetengeneza bidhaa tatu?Question 18
- Ni nani hakuandamana na wenzake kupeleka bidhaa sokoni?Question 19
- Ni kauli ipi inayoeleza waliochonga vinyago kwa mujibu wa kifungu?Question 20
- Tiro alimsalimia babu yake kwa kusema “Habari gani?” Je, ni salamu gani nyingine angeweza kutumia kumwamkua?Question 21
- Ni methali gani inayofaa kujaza nafasi katika kifungu?Question 22