CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 22
Ni methali gani inayofaa kujaza nafasi katika kifungu?
From Kiswahili Paper 1 — October 2026 Collection · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa kusoma
(Ni asubuhi. Tiro amekutana na babu yake njiani akielekea dukani. Tiro anamnyoshea mkono kumwamkua.)
Tiro: (Kwa furaha) Babu, habari gani?
Babu: (Akitabasamu) Njema mjukuu wangu. Unaelekea wapi asubuhi hii?
Tiro: Nimetumwa dukani kununua maziwa ya kupikia chai.
Babu: Ah! Kijana mwadilifu kwelikweli, ukitumwa nenda. Usikatae. Hayo ndiyo maadili, mjukuu wangu.
Tiro: Nashukuru babu. Je, ng’ombe wako amezaa?
Babu: (Kwa huzuni) La! Mjukuu wangu, yule ng’ombe aliugua na akafa. Hata hivyo, Waswahili husema, __________.
Tiro: (Kwa uchangamfu) Usiwe na shaka. Wale ng’ombe wengine waliobaki watakuzalia. ________. Hizo ni changamoto za ufugaji.
Babu: (Akitikisa kichwa kukubaliana naye) Umegonga ndipo mjukuu wangu.
Tiro: (Akimsikiliza) Najua wewe ni mfugaji hodari. Sasa wacha nikimbie dukani nisicheleweshe mama kutuandalia kiamsha kinywa.

- ANguzo moja haijengi nyumba.
- BAjizi ni nyumba ya njaa.
- CKwendako hisani hurudi.
- DKuvunjika kwa mwiko si mwisho wa kusonga ugali.
Answer
D. Kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa kusonga ugali.
Methali hiyo inaonyesha kuwa kupoteza ng’ombe mmoja hakumalizi uwezo wa kuendelea na ufugaji.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Ni tabia gani haikuonyeshwa katika mazungumzo haya?Question 23
- Chagua nahau inayofaa kujaza nafasi katika kifungu.Question 24
- Ni methali ipi inayofaa kuelezea maneno ya Tiro kuhusu changamoto za ufugaji?Question 25
- Chagua jibu linalofaa kwa nafasi ya 26.Question 26
- Chagua jibu linalofaa kwa nafasi ya 27.Question 27
- Chagua jibu linalofaa kwa nafasi ya 28.Question 28