CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 21
Tiro alimsalimia babu yake kwa kusema “Habari gani?” Je, ni salamu gani nyingine angeweza kutumia kumwamkua?
From Kiswahili Paper 1 — October 2026 Collection · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa kusoma
(Ni asubuhi. Tiro amekutana na babu yake njiani akielekea dukani. Tiro anamnyoshea mkono kumwamkua.)
Tiro: (Kwa furaha) Babu, habari gani?
Babu: (Akitabasamu) Njema mjukuu wangu. Unaelekea wapi asubuhi hii?
Tiro: Nimetumwa dukani kununua maziwa ya kupikia chai.
Babu: Ah! Kijana mwadilifu kwelikweli, ukitumwa nenda. Usikatae. Hayo ndiyo maadili, mjukuu wangu.
Tiro: Nashukuru babu. Je, ng’ombe wako amezaa?
Babu: (Kwa huzuni) La! Mjukuu wangu, yule ng’ombe aliugua na akafa. Hata hivyo, Waswahili husema, __________.
Tiro: (Kwa uchangamfu) Usiwe na shaka. Wale ng’ombe wengine waliobaki watakuzalia. ________. Hizo ni changamoto za ufugaji.
Babu: (Akitikisa kichwa kukubaliana naye) Umegonga ndipo mjukuu wangu.
Tiro: (Akimsikiliza) Najua wewe ni mfugaji hodari. Sasa wacha nikimbie dukani nisicheleweshe mama kutuandalia kiamsha kinywa.
Tiro: (Kwa furaha) Babu, habari gani?
Babu: (Akitabasamu) Njema mjukuu wangu. Unaelekea wapi asubuhi hii?
Tiro: Nimetumwa dukani kununua maziwa ya kupikia chai.
Babu: Ah! Kijana mwadilifu kwelikweli, ukitumwa nenda. Usikatae. Hayo ndiyo maadili, mjukuu wangu.
Tiro: Nashukuru babu. Je, ng’ombe wako amezaa?
Babu: (Kwa huzuni) La! Mjukuu wangu, yule ng’ombe aliugua na akafa. Hata hivyo, Waswahili husema, __________.
Tiro: (Kwa uchangamfu) Usiwe na shaka. Wale ng’ombe wengine waliobaki watakuzalia. ________. Hizo ni changamoto za ufugaji.
Babu: (Akitikisa kichwa kukubaliana naye) Umegonga ndipo mjukuu wangu.
Tiro: (Akimsikiliza) Najua wewe ni mfugaji hodari. Sasa wacha nikimbie dukani nisicheleweshe mama kutuandalia kiamsha kinywa.
Tiro alimsalimia babu yake kwa kusema “Habari gani?” Je, ni salamu gani nyingine angeweza kutumia kumwamkua?
- ASabalkheri?
- BShikamoo?
- CWaambaje?
- DSalaam aleikum?
Answer
B. Shikamoo?
Shikamoo ni salamu ya heshima inayotumiwa na mdogo kumwamkua mkubwa.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Ni methali gani inayofaa kujaza nafasi katika kifungu?Question 22
- Ni tabia gani haikuonyeshwa katika mazungumzo haya?Question 23
- Chagua nahau inayofaa kujaza nafasi katika kifungu.Question 24
- Ni methali ipi inayofaa kuelezea maneno ya Tiro kuhusu changamoto za ufugaji?Question 25
- Chagua jibu linalofaa kwa nafasi ya 26.Question 26
- Chagua jibu linalofaa kwa nafasi ya 27.Question 27