naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 24

Chagua nahau inayofaa kujaza nafasi katika kifungu.

From Kiswahili Paper 1 — October 2026 Collection · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa kusoma

(Ni asubuhi. Tiro amekutana na babu yake njiani akielekea dukani. Tiro anamnyoshea mkono kumwamkua.)
Tiro: (Kwa furaha) Babu, habari gani?
Babu: (Akitabasamu) Njema mjukuu wangu. Unaelekea wapi asubuhi hii?
Tiro: Nimetumwa dukani kununua maziwa ya kupikia chai.
Babu: Ah! Kijana mwadilifu kwelikweli, ukitumwa nenda. Usikatae. Hayo ndiyo maadili, mjukuu wangu.
Tiro: Nashukuru babu. Je, ng’ombe wako amezaa?
Babu: (Kwa huzuni) La! Mjukuu wangu, yule ng’ombe aliugua na akafa. Hata hivyo, Waswahili husema, __________.
Tiro: (Kwa uchangamfu) Usiwe na shaka. Wale ng’ombe wengine waliobaki watakuzalia. ________. Hizo ni changamoto za ufugaji.
Babu: (Akitikisa kichwa kukubaliana naye) Umegonga ndipo mjukuu wangu.
Tiro: (Akimsikiliza) Najua wewe ni mfugaji hodari. Sasa wacha nikimbie dukani nisicheleweshe mama kutuandalia kiamsha kinywa.

Chagua nahau inayofaa kujaza nafasi katika kifungu.

  1. AJipe moyo.
  2. BKata tamaa.
  3. CVunja moyo.
  4. DAka!

Answer

A. Jipe moyo.

Jipe moyo ni kujitia matumaini na ujasiri wakati wa changamoto.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test