CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 25
Ni methali ipi inayofaa kuelezea maneno ya Tiro kuhusu changamoto za ufugaji?
From Kiswahili Paper 1 — October 2026 Collection · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa kusoma
(Ni asubuhi. Tiro amekutana na babu yake njiani akielekea dukani. Tiro anamnyoshea mkono kumwamkua.)
Tiro: (Kwa furaha) Babu, habari gani?
Babu: (Akitabasamu) Njema mjukuu wangu. Unaelekea wapi asubuhi hii?
Tiro: Nimetumwa dukani kununua maziwa ya kupikia chai.
Babu: Ah! Kijana mwadilifu kwelikweli, ukitumwa nenda. Usikatae. Hayo ndiyo maadili, mjukuu wangu.
Tiro: Nashukuru babu. Je, ng’ombe wako amezaa?
Babu: (Kwa huzuni) La! Mjukuu wangu, yule ng’ombe aliugua na akafa. Hata hivyo, Waswahili husema, __________.
Tiro: (Kwa uchangamfu) Usiwe na shaka. Wale ng’ombe wengine waliobaki watakuzalia. ________. Hizo ni changamoto za ufugaji.
Babu: (Akitikisa kichwa kukubaliana naye) Umegonga ndipo mjukuu wangu.
Tiro: (Akimsikiliza) Najua wewe ni mfugaji hodari. Sasa wacha nikimbie dukani nisicheleweshe mama kutuandalia kiamsha kinywa.

- ANguzo moja haijengi nyumba.
- BAjizi ni nyumba ya njaa.
- CKwendako hisani hurudi.
- DKuvunjika kwa mwiko si mwisho wa kusonga ugali.
Answer
D. Kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa kusonga ugali.
Tiro anaeleza kwamba changamoto moja haimalizi ufugaji; hilo linaafikiana na kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa kusonga ugali.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Chagua jibu linalofaa kwa nafasi ya 26.Question 26
- Chagua jibu linalofaa kwa nafasi ya 27.Question 27
- Chagua jibu linalofaa kwa nafasi ya 28.Question 28
- Chagua jibu linalofaa kwa nafasi ya 29.Question 29
- Chagua jibu linalofaa kwa nafasi ya 30.Question 30
- Chagua jibu linalofaa kwa nafasi ya 31.Question 31