naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 15

Kifungu hiki kimebainisha kuwa visa vya ubakaji hutokea kwa sababu ya:

From Kiswahili Paper 1 — October 2026 Collection · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa kusoma

Unyanyasaji wa kijinsia ni jambo lililopitwa na wakati. Kinyume na hali ilivyo sasa, jamii nyingi zimeona mwanga. Baadhi ya wanaojihusisha na vitendo hivi hujikuta mashakani. Uvundo uliozagaa na kukithiri katika jamii kutokana na vitendo hivi hudhihirisha udhalilishaji wa jinsia.
Aghalabu, ni watu wanaojulikana katika jamii ndio wanaojihusisha na vitendo hivi. Ukweli ni kuwa binadamu hawapaswi kudhalilishana. Visa vya ubakaji havitokani na sababu moja tu, bali hutokana na unyama ulio ndani ya mbakaji. Hiki ni kitendo cha aibu, na athari zake ni mbaya sana kwa wahanga. Baadhi hupata magonjwa ya zinaa na wengine hupoteza maisha mikononi mwa wahalifu.
Jambo la kusikitisha ni kuwa vitendo hivi vya kinyama hutekelezwa na watu wanaojulikana katika jamii. Vyaweza kutokea nyumbani, kazini, njiani na hata mitaani. Shime jamani! Tuungane sote ili tuweze kukomesha unyanyasaji wa aina yoyote wa kijinsia. Vijana, wazee, wazazi na jamii kwa jumla, ni jukumu letu kukabili maovu haya. Tuache utashi wa moyo na tuwasaidie wenzetu wanaokabiliwa na vitendo hivi viovu.

Kifungu hiki kimebainisha kuwa visa vya ubakaji hutokea kwa sababu ya:

  1. AWivu na tamaa.
  2. BUnyama ulio ndani ya mbakaji.
  3. CTamaa na uwajibikaji.
  4. DKutowajibika na tamaa.

Answer

B. Unyama ulio ndani ya mbakaji.

Kifungu kinahusisha ubakaji na unyama wa mbakaji; hakihusishi kosa hilo na tabia za mhanga.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test