naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 14

Ni jawabu gani lililo sahihi kwa mujibu wa kifungu?

From Kiswahili Paper 1 — October 2026 Collection · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa kusoma

Unyanyasaji wa kijinsia ni jambo lililopitwa na wakati. Kinyume na hali ilivyo sasa, jamii nyingi zimeona mwanga. Baadhi ya wanaojihusisha na vitendo hivi hujikuta mashakani. Uvundo uliozagaa na kukithiri katika jamii kutokana na vitendo hivi hudhihirisha udhalilishaji wa jinsia.
Aghalabu, ni watu wanaojulikana katika jamii ndio wanaojihusisha na vitendo hivi. Ukweli ni kuwa binadamu hawapaswi kudhalilishana. Visa vya ubakaji havitokani na sababu moja tu, bali hutokana na unyama ulio ndani ya mbakaji. Hiki ni kitendo cha aibu, na athari zake ni mbaya sana kwa wahanga. Baadhi hupata magonjwa ya zinaa na wengine hupoteza maisha mikononi mwa wahalifu.
Jambo la kusikitisha ni kuwa vitendo hivi vya kinyama hutekelezwa na watu wanaojulikana katika jamii. Vyaweza kutokea nyumbani, kazini, njiani na hata mitaani. Shime jamani! Tuungane sote ili tuweze kukomesha unyanyasaji wa aina yoyote wa kijinsia. Vijana, wazee, wazazi na jamii kwa jumla, ni jukumu letu kukabili maovu haya. Tuache utashi wa moyo na tuwasaidie wenzetu wanaokabiliwa na vitendo hivi viovu.

Ni jawabu gani lililo sahihi kwa mujibu wa kifungu?

  1. ANi watoto wa kike pekee ambao hubakwa na kunajisiwa.
  2. BUbakaji na unajisi hufanyika sehemu za siri pekee.
  3. CWanaonyanyasa watu kingono aghalabu ni watu wanaojulikana.
  4. DTabia za mtu zaweza kumfanya kubakwa.

Answer

C. Wanaonyanyasa watu kingono aghalabu ni watu wanaojulikana.

Kifungu kinasema aghalabu wanaotekeleza vitendo hivi ni watu wanaojulikana katika jamii.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test