naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 1

Mazungumzo haya yamefanyika wakati gani?

From Test 18 — Lugha: Formative Assessment 2026 · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Mazungumzo
Tina: (Kwa furaha) Sabalheri sahibu?
Rita: Aheri rafiki yangu. Habari za nyumbani?
Tina: Nzuri ndugu yangu. Umenipotelea siku nyingi. Umekuwa wapi?
Rita: Nimekuwa nikimtunza nyanya nyumbani kwake. Ameugua kwa muda mrefu sana.
Tina: Pole sana dada. Je, amepata afueni?
Rita: (Akidondokwa na machozi) La! Nyanya aliipungia dunia mkono wa buriani juzi. Kwa sasa, mipango ya mazishi yake imeshika kazi.
Tina: (Akimfariji na kumkumbatia) Kwa mara nyingine tena, pokea pole zangu. Mungu awahurumie.

Mazungumzo haya yamefanyika wakati gani?

  1. AAsubuhi
  2. BMchana
  3. CJioni
  4. DUsiku

Answer

A. Asubuhi

Tina anamsalimia Rita kwa 'Sabalheri', salamu ya asubuhi, na Rita anajibu kwa 'Aheri' -- jozi hii ya salamu hutumika asubuhi pekee, hivyo mazungumzo yalifanyika asubuhi.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test