naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 3

Ikiwa juzi ilikuwa Jumamosi, Rita na Tina walikutana siku gani?

From Test 18 — Lugha: Formative Assessment 2026 · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Mazungumzo
Tina: (Kwa furaha) Sabalheri sahibu?
Rita: Aheri rafiki yangu. Habari za nyumbani?
Tina: Nzuri ndugu yangu. Umenipotelea siku nyingi. Umekuwa wapi?
Rita: Nimekuwa nikimtunza nyanya nyumbani kwake. Ameugua kwa muda mrefu sana.
Tina: Pole sana dada. Je, amepata afueni?
Rita: (Akidondokwa na machozi) La! Nyanya aliipungia dunia mkono wa buriani juzi. Kwa sasa, mipango ya mazishi yake imeshika kazi.
Tina: (Akimfariji na kumkumbatia) Kwa mara nyingine tena, pokea pole zangu. Mungu awahurumie.

Ikiwa juzi ilikuwa Jumamosi, Rita na Tina walikutana siku gani?

  1. AJumapili
  2. BJumanne
  3. CJumatano
  4. DJumatatu

Answer

D. Jumatatu

Rita anasema nyanya aliaga dunia 'juzi'. Ikiwa juzi (siku mbili kabla ya leo) ilikuwa Jumamosi, basi jana ilikuwa Jumapili na leo (siku ya mazungumzo) ni Jumatatu.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test