naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 4

Chagua kauli sahihi kulingana na mazungumzo:

From Test 18 — Lugha: Formative Assessment 2026 · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Mazungumzo
Tina: (Kwa furaha) Sabalheri sahibu?
Rita: Aheri rafiki yangu. Habari za nyumbani?
Tina: Nzuri ndugu yangu. Umenipotelea siku nyingi. Umekuwa wapi?
Rita: Nimekuwa nikimtunza nyanya nyumbani kwake. Ameugua kwa muda mrefu sana.
Tina: Pole sana dada. Je, amepata afueni?
Rita: (Akidondokwa na machozi) La! Nyanya aliipungia dunia mkono wa buriani juzi. Kwa sasa, mipango ya mazishi yake imeshika kazi.
Tina: (Akimfariji na kumkumbatia) Kwa mara nyingine tena, pokea pole zangu. Mungu awahurumie.

Chagua kauli sahihi kulingana na mazungumzo:

  1. ARita na Tina walikuwa wakikutana mara kwa mara
  2. BRita alidondokwa na machozi kwa kuwa Tina hakujua yaliyompata
  3. CMaradhi aliyougua nyanya yaliwatenganisha marafiki hawa kwa muda
  4. DWazazi wa Tina walijua kuhusu kifo cha nyanya

Answer

C. Maradhi aliyougua nyanya yaliwatenganisha marafiki hawa kwa muda

Rita anaeleza 'Nimekuwa nikimtunza nyanya nyumbani kwake. Ameugua kwa muda mrefu sana' -- hii inaeleza kwamba ugonjwa wa nyanya ndio uliomfanya Rita na Tina wasikutane kwa muda ('umenipotelea siku nyingi').

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test