naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 2

Mapafu hufanya kazi gani katika mwili wa binadamu kulingana na mazungumzo haya?

From Test 12 — Grade 6 Revision 2, 2026 (Shughuli za Kiswahili) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Daktari: Habari za alasiri binti? Karibu sana kwenye hospitali ya Tiba bora.
Nyumbura: Sijambo daktari. Nimekutembelea kwa sababu sihisi vyema kabisa kwenye mapafu yangu.
Daktari: Maskini! Pole sana kwa jinsi unavyosikia. Unahisi vipi? Umeanza kuhisi hivyo tangu lini?
Nyumbura: Nimekuwa na maumivu makali ya mapafu, ninapopumua usiku napata shida sana. Muda mwingine nahisi baridi na uchungu hasa ninapokohoa.
Daktari: Pole sana binti. Nitakuchunguza kisha niweze kutambua hasa chanzo cha hali yako. Usiku huwa unahisi joto?
Nyumbura: Naam, huwa ninapata joto jingi usiku. Isitoshe, kuna muda nahisi uchovu mwingi mwilini.
Daktari: Haya hebu nikupime joto kisha niangalie mapigo ya moyo. Inaonekana kifua chako ili tujue hali halisi.
Nyumbura: Naweza kuwa na kifua kikuu?
Daktari: Sina hakika, tusubiri kwanza tufanye vipimo kisha tutajua ukweli. Vipimo hivi vitatufahamisha ni nini hasa kinachokuuma kisha tutaweza kukutibu.
Nyumbura: Shukran sana daktari. Nimeshukuru na wema wako.

Mapafu hufanya kazi gani katika mwili wa binadamu kulingana na mazungumzo haya?

  1. AHusafisha damu
  2. BHusafisha hewa
  3. CHusaga chakula
  4. DHudhibiti viwango vya sukari

Answer

B. Husafisha hewa

Nyumbura analalamikia maumivu ya mapafu anapopumua -- mapafu ni kiungo kinachotumika katika kupumua, yaani kusafisha na kubadilishana hewa mwilini, si kusafisha damu, kusaga chakula wala kudhibiti sukari.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test