CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 8
Kifungu kinasema kuwa masomo yanaweza kumpatia mtu nini?
From Test 12 — Grade 6 Revision 2, 2026 (Shughuli za Kiswahili) · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu
Kifungu cha ufahamu: Umaskini (maswali 6-10)
Umaskini ni hali ya kukosa mali au pesa ambayo inampelekea mtu kukosa kuweza kukidhi mahitaji yake ya kimsingi pamoja na wale ambao wanamtegemea. Hali hii humfanya mtu akose kuwa na mavazi mazuri, chakula cha kutosha, makazi na hata kukosa kujiendeleza kielimu. Mtu ambaye ni maskini huwa hana uwezo wa kujiamulia mambo mengi hasa yanayohitaji uwezo wa fedha.
Mtu anaweza kujitoa katika hali ya umaskini kwa kufanya biashara akitumia pesa na baadaye apate faida. Faida hutumiwa kununua na kulipia bidhaa muhimu katika maisha. Hata hivyo, ikiwa mtu huyo hatatumia pesa vizuri, anaweza kupata hasara.
Mbali na biashara, mtu anaweza kusoma na kupata ujuzi ambao utampatia ajira na njia za kujitegemea mbeleni. Akiwa kazini anaweza kulipwa mshahara mwishoni mwa kila mwezi. Malipo haya anaweza kuyatumia kulipia gharama za maisha pamoja na kuwekea akiba kidogo. Akiba humsaidia mtu wakati ambapo ameishiwa na kipato na kuna dharura.
Baadhi ya watu hujihusisha katika kilimo. Wanaweza kupanda mazao ama kufuga wanyama kama vile ng'ombe na mbuzi na kupata faida kemkem. Wanyama hawa huuzwa na kuleta faida kwa wafugaji. Ni vyema kila mmoja kushiriki katika shughuli za kiuchumi ambazo zinasaidia kupiga teke umaskini na kumfanya kila mmoja kuweza kuishi maisha yanayostahili.

- APesa za kufaulu katika maisha
- BFaida katika biashara
- CHasara ikiwa biashara haitafanikiwa
- DUjuzi wa kuweza kujitoa katika umaskini
Answer
D. Ujuzi wa kuweza kujitoa katika umaskini
Kifungu kinasema mtu anaweza kusoma na kupata ujuzi utakaompatia ajira na njia za kujitegemea, yaani kujitoa katika umaskini -- si pesa za moja kwa moja, faida ya biashara, wala hasara.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Mtu akiishiwa na pesa zake ama awe na dharura anaweza kupata msaada kutoka kwa?Question 9
- Ni ipi miongoni mwa hizi si shughuli ya kiuchumi ambayo inaweza kumfaa mtu?Question 10
- Shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti kama hili huitwa?Question 11
- Mshairi anazungumzia jambo gani katika shairi hili?Question 12
- Kibwagizo cha shairi hili kinasema kuwaQuestion 13
- Shairi hili lote lina mishororo mingapi?Question 14