naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 11

Shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti kama hili huitwa?

From Test 12 — Grade 6 Revision 2, 2026 (Shughuli za Kiswahili) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ushairi

Shairi: Mazingira Tuyalinde (maswali 11-15)
Leo nawaelezeni, msikilize vizuri,
Nisemayo yashikeni, nataka niyakariri,
Wa bara na hata mijini, nawaeleza dhahiri,
Mazingira tuyalinde, yasichafuke daima.

Mito yetu kuchafua, si jambo lenye faida,
Mito ni maji tambua, kesho tusilete shida,
Maziwa yetu na mvua, tulinde kaka na dada,
Mazingira tuyalinde, yasichafuke daima.

Mwisho ninamalizia, hewa nayo tuitunze,
Misitu na miti pia, kuitunza tujifunze,
Udongo unapopitia, usiende tuukinze,
Mazingira tuyalinde, yasichafuke daima.

Shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti kama hili huitwa?

  1. ATathlitha
  2. BTakhmisa
  3. CTarbia
  4. DTahnia

Answer

C. Tarbia

Shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti huitwa tarbia; tathlitha huwa na mishororo mitatu na takhmisa huwa na mishororo mitano kwa kila ubeti.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test