CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 12
Mshairi anazungumzia jambo gani katika shairi hili?
From Test 12 — Grade 6 Revision 2, 2026 (Shughuli za Kiswahili) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ushairi
Shairi: Mazingira Tuyalinde (maswali 11-15)
Leo nawaelezeni, msikilize vizuri,
Nisemayo yashikeni, nataka niyakariri,
Wa bara na hata mijini, nawaeleza dhahiri,
Mazingira tuyalinde, yasichafuke daima.
Mito yetu kuchafua, si jambo lenye faida,
Mito ni maji tambua, kesho tusilete shida,
Maziwa yetu na mvua, tulinde kaka na dada,
Mazingira tuyalinde, yasichafuke daima.
Mwisho ninamalizia, hewa nayo tuitunze,
Misitu na miti pia, kuitunza tujifunze,
Udongo unapopitia, usiende tuukinze,
Mazingira tuyalinde, yasichafuke daima.
Leo nawaelezeni, msikilize vizuri,
Nisemayo yashikeni, nataka niyakariri,
Wa bara na hata mijini, nawaeleza dhahiri,
Mazingira tuyalinde, yasichafuke daima.
Mito yetu kuchafua, si jambo lenye faida,
Mito ni maji tambua, kesho tusilete shida,
Maziwa yetu na mvua, tulinde kaka na dada,
Mazingira tuyalinde, yasichafuke daima.
Mwisho ninamalizia, hewa nayo tuitunze,
Misitu na miti pia, kuitunza tujifunze,
Udongo unapopitia, usiende tuukinze,
Mazingira tuyalinde, yasichafuke daima.
Mshairi anazungumzia jambo gani katika shairi hili?
- AUmuhimu wa maji
- BUmuhimu wa kutunza mazingira
- CUmuhimu wa mashairi
- DUmuhimu wa beti
Answer
B. Umuhimu wa kutunza mazingira
Kila ubeti unamalizika kwa wimbo-rudufu "Mazingira tuyalinde, yasichafuke daima", na mshairi anataja mito, hewa, misitu na udongo -- vyote ni sehemu za mazingira, kwa hivyo dhamira kuu ni umuhimu wa kutunza mazingira, si maji peke yake.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Kibwagizo cha shairi hili kinasema kuwaQuestion 13
- Shairi hili lote lina mishororo mingapi?Question 14
- Ni sehemu gani ya mazingira ambayo haijatajwa na mshairi?Question 15
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi (16).Question 16
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi (17).Question 17
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi (18).Question 18