naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 6

Kulingana na ufahamu ni kweli kusema kuwa.

From Test 12 — Grade 6 Revision 2, 2026 (Shughuli za Kiswahili) · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Kifungu cha ufahamu: Umaskini (maswali 6-10)
Umaskini ni hali ya kukosa mali au pesa ambayo inampelekea mtu kukosa kuweza kukidhi mahitaji yake ya kimsingi pamoja na wale ambao wanamtegemea. Hali hii humfanya mtu akose kuwa na mavazi mazuri, chakula cha kutosha, makazi na hata kukosa kujiendeleza kielimu. Mtu ambaye ni maskini huwa hana uwezo wa kujiamulia mambo mengi hasa yanayohitaji uwezo wa fedha.

Mtu anaweza kujitoa katika hali ya umaskini kwa kufanya biashara akitumia pesa na baadaye apate faida. Faida hutumiwa kununua na kulipia bidhaa muhimu katika maisha. Hata hivyo, ikiwa mtu huyo hatatumia pesa vizuri, anaweza kupata hasara.

Mbali na biashara, mtu anaweza kusoma na kupata ujuzi ambao utampatia ajira na njia za kujitegemea mbeleni. Akiwa kazini anaweza kulipwa mshahara mwishoni mwa kila mwezi. Malipo haya anaweza kuyatumia kulipia gharama za maisha pamoja na kuwekea akiba kidogo. Akiba humsaidia mtu wakati ambapo ameishiwa na kipato na kuna dharura.

Baadhi ya watu hujihusisha katika kilimo. Wanaweza kupanda mazao ama kufuga wanyama kama vile ng'ombe na mbuzi na kupata faida kemkem. Wanyama hawa huuzwa na kuleta faida kwa wafugaji. Ni vyema kila mmoja kushiriki katika shughuli za kiuchumi ambazo zinasaidia kupiga teke umaskini na kumfanya kila mmoja kuweza kuishi maisha yanayostahili.

Kulingana na ufahamu ni kweli kusema kuwa.

  1. AKila mtu asiyekuwa na mali mengi hana chakula na mavazi
  2. BMasikini huwa hawawezi kupata mali na pesa
  3. CMtu asiyekuwa na mali na pesa hupata huduma za kimsingi kwa shida
  4. DMasikini wengine wana mali na pesa lakini hawana elimu

Answer

C. Mtu asiyekuwa na mali na pesa hupata huduma za kimsingi kwa shida

Kifungu kinasema umaskini humfanya mtu akose mavazi mazuri, chakula cha kutosha, makazi na elimu -- yaani huduma za kimsingi hupatikana kwa shida, si kwamba haziwezekani kabisa (A ni jumla kupita kiasi, B na D hazitajwi kifunguni).

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test