naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 8

Bila kutumia kamusi, tambua neno lenye maana sawa na neno "tabasamu."

From Test 1 — Endterm 3 Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Msamiati

Mwaka uliopita, sherehe ya kufunga mwaka iliandaliwa nyumbani kwetu. Asubuhi hiyo, hema kubwa lilikuwa limewekwa katika uga wa nyumba yetu. Viti vya kupendeza vilipangwa kuzunguka meza.

Majirani, jamaa na marafiki walioalikwa waliingia na kuketi kwenye viti ndani ya hema. Nyuso zao ziling'aa kwa tabasamu. Siku njema huonekana asubuhi.

Sherehe ilianza saa tatu unusu. Mama aliwakaribisha wote na kusema, "Ndugu zangu, ni furaha kubwa kukutana tena katika kipindi hiki. Leo hii nina furaha kuwajulisha kuwa Johana, mwana wa Bi. Wakesho, pamoja na mpenzi wake, Johari, wanatualika sote katika harusi itakayofanyika mwezi ujao. Ninajua tutaungana kuwapiga jeki. Ndugu ni kufaana."

Baada ya hayo, mama alimkaribisha babu ambaye alitupa ushauri wa busara kwamba umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Watoto walishauriwa kwenda kucheza huku watu wazima wakishiriki maongezi. Sherehe iliisha mwendo wa saa tisa alasiri.

Bila kutumia kamusi, tambua neno lenye maana sawa na neno "tabasamu."

  1. Afuraha
  2. Bcheka
  3. Cnuna
  4. Dpenda

Answer

B. cheka

"Tabasamu" (kutabasamu) ni kitendo cha kuonyesha furaha usoni kwa kutoa mwonekano kama anayecheka kidogo -- "cheka" ndilo neno lenye maana sawa zaidi na "tabasamu" miongoni mwa majibu yaliyotolewa.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test