naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 10

Tambua jibu linaloonyesha mfuatano wa matukio namna yalivyojitokeza katika kifungu.

From Test 1 — Endterm 3 Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Mwaka uliopita, sherehe ya kufunga mwaka iliandaliwa nyumbani kwetu. Asubuhi hiyo, hema kubwa lilikuwa limewekwa katika uga wa nyumba yetu. Viti vya kupendeza vilipangwa kuzunguka meza.

Majirani, jamaa na marafiki walioalikwa waliingia na kuketi kwenye viti ndani ya hema. Nyuso zao ziling'aa kwa tabasamu. Siku njema huonekana asubuhi.

Sherehe ilianza saa tatu unusu. Mama aliwakaribisha wote na kusema, "Ndugu zangu, ni furaha kubwa kukutana tena katika kipindi hiki. Leo hii nina furaha kuwajulisha kuwa Johana, mwana wa Bi. Wakesho, pamoja na mpenzi wake, Johari, wanatualika sote katika harusi itakayofanyika mwezi ujao. Ninajua tutaungana kuwapiga jeki. Ndugu ni kufaana."

Baada ya hayo, mama alimkaribisha babu ambaye alitupa ushauri wa busara kwamba umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Watoto walishauriwa kwenda kucheza huku watu wazima wakishiriki maongezi. Sherehe iliisha mwendo wa saa tisa alasiri.

Tambua jibu linaloonyesha mfuatano wa matukio namna yalivyojitokeza katika kifungu.

  1. AWatoto kucheza, babu na mama kutoa hotuba, watu kukusanyika, sherehe kukamilika.
  2. BWatu kukusanyika, mama na babu kutoa hotuba, watoto kucheza, sherehe kukamilika.
  3. CMama na babu kutoa hotuba, watoto kucheza, sherehe kukamilika, watu kukusanyika.
  4. DBabu na mama kutoa hotuba.

Answer

B. Watu kukusanyika, mama na babu kutoa hotuba, watoto kucheza, sherehe kukamilika.

Kifungu kinaonyesha watu wakikusanyika kwanza, kisha mama na babu wakitoa hotuba, kisha watoto wakienda kucheza, na mwishowe sherehe kukamilika.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test