CBC Grade 6 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 7
Kulingana na kifungu, Johana na Johari walifanya harusi mwezi gani?
From Test 1 — Endterm 3 Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu
Mwaka uliopita, sherehe ya kufunga mwaka iliandaliwa nyumbani kwetu. Asubuhi hiyo, hema kubwa lilikuwa limewekwa katika uga wa nyumba yetu. Viti vya kupendeza vilipangwa kuzunguka meza.
Majirani, jamaa na marafiki walioalikwa waliingia na kuketi kwenye viti ndani ya hema. Nyuso zao ziling'aa kwa tabasamu. Siku njema huonekana asubuhi.
Sherehe ilianza saa tatu unusu. Mama aliwakaribisha wote na kusema, "Ndugu zangu, ni furaha kubwa kukutana tena katika kipindi hiki. Leo hii nina furaha kuwajulisha kuwa Johana, mwana wa Bi. Wakesho, pamoja na mpenzi wake, Johari, wanatualika sote katika harusi itakayofanyika mwezi ujao. Ninajua tutaungana kuwapiga jeki. Ndugu ni kufaana."
Baada ya hayo, mama alimkaribisha babu ambaye alitupa ushauri wa busara kwamba umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Watoto walishauriwa kwenda kucheza huku watu wazima wakishiriki maongezi. Sherehe iliisha mwendo wa saa tisa alasiri.

- AMwezi ujao
- BDisemba
- CJulai
- DJanuari
Answer
A. Mwezi ujao
Mama anasema harusi "itakayofanyika mwezi ujao."
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Bila kutumia kamusi, tambua neno lenye maana sawa na neno "tabasamu."Question 8
- Ni methali gani iliyotumika katika kifungu inayoonyesha umuhimu wa ushirikiano?Question 9
- Tambua jibu linaloonyesha mfuatano wa matukio namna yalivyojitokeza katika kifungu.Question 10
- Miwa ni mimeaQuestion 11
- Baadhi ya maradhi yanayoweza kuzuiwa na sharubati ya miwa niQuestion 12
- Chagua jibu sahihi.Question 13