naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 14

Kwa nini wanafunzi walishauriwa kunywa maji mengi?

From Kiswahili — End Term 1 Assessment 2025 (Set 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 8 hadi la 14.
Mwaka huu ulipoanza, sote tulifurahi kurudi katika shule yetu. Shule hiyo inajulikana kama Mematele. Ina wanafunzi elfu moja na mia mbili na mabasi sita. Mabasi yote ya shule hiyo yamepakwa rangi ya manjano.
Tulipowasili shuleni, tuliingia madarasani na kuketi kwenye viti vyetu. Mwalimu mmoja ambaye tulimpenda sana aliingia darasani na kutuamkua, "Hamjambo wanafunzi?" Nasi tukajibu, "Hatujambo mwalimu Matunda. Shikamoo."
Kengele ilipopigwa tulielekea gwarideni. Tulisimama wima tulipokuwa tukiimba wimbo wa taifa. Baadaye mwalimu alitukagua endapo kucha zetu zilikuwa safi. Mwalimu wetu alitushauri tuwe tukinywa maji mengi kila siku ili tuwe na afya njema.

14. Kwa nini wanafunzi walishauriwa kunywa maji mengi?

Answer

Ili wawe na afya njema.

"ili tuwe na afya njema".

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test