naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 7

Ni haki ngapi za watoto zimetajwa kwenye kifungu ulichokisoma?

From Kiswahili — End of Year Assessment 2026 (Set 15) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.
Kulingana na Katiba mpya ya Kenya, mtoto ni mtu yeyote aliye chini ya umri wa miaka kumi na minane. Mambo ambayo kila mtoto anapaswa kupewa au kupata huitwa haki za watoto.
Baadhi ya haki hizo ni kama vile kupata malezi bora, matibabu, elimu, chakula na ulinzi, pamoja na kulindwa kutokana na dhuluma zozote zile. Mtoto anapodhulumiwa anapaswa kuripoti kwa mlezi wake, polisi, mwalimu au yeyote katika jamii anayeweza kumpa usaidizi.
Baadhi ya dhuluma hizo ni kunajisiwa, kukeketwa kwa wasichana, kunyimwa chakula na kadhalika. Mtoto naye anastahili kuwaheshimu watu wote katika jamii.

7. Ni haki ngapi za watoto zimetajwa kwenye kifungu ulichokisoma?

  1. A8
  2. B6
  3. C2
  4. D4

Answer

B. 6

Malezi bora, matibabu, elimu, chakula, ulinzi na kulindwa kutokana na dhuluma: haki sita.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test