CBC Grade 5 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 13
Kwa nini Hassan alienda nyumbani?
From Kiswahili — End of Year Assessment 2026 (Set 15) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali.
Siku moja Hassan alirudi nyumbani kwao mapema kuliko kawaida yake. Jambo hili lilifanyika kwa sababu alikuwa akihisi uchungu mwingi tumboni. Alipoenda hospitalini, daktari alimtibu na kumwambia aende nyumbani ajipumzishe ili maumivu yatulie. Alikuwa amekunywa maji yenye viini hatari.
Alipokaribia lango la kuingia kwao, alisikia sauti ikitoka kwenye zizi. Alitaka kujua yaliyokuwa yakijiri. Alipofika pale zizini, alipigwa na butwaa kwa yale aliyoyaona. Alikuta jirani yao Pwagu akimkama ng'ombe wao. Alipiga mayowe yaliyovutia majirani. Pwagu alikamatwa na kupelekwa kwenye ofisi ya chifu.
13. Kwa nini Hassan alienda nyumbani?
- AIli amkamate mwizi zizini
- BIli aende hospitalini
- CAlikuwa ameamriwa na daktari akapumzike nyumbani
- DAlikuwa na njaa
Answer
C. Alikuwa ameamriwa na daktari akapumzike nyumbani
Daktari alimwambia aende nyumbani ajipumzishe.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Maneno “alipigwa na butwaa” kama yalivyotumiwa katika kifungu yana maana gani?Question 14
- Ni methali gani inayoafikiana na kifungu ulichokisoma?Question 15
- Chagua jibu sahihi la pengo la 16.Question 16
- Chagua jibu sahihi la pengo la 17.Question 17
- Chagua jibu sahihi la pengo la 18.Question 18
- Chagua jibu sahihi la pengo la 19.Question 19