CBC Grade 5 Kiswahili End Term 3 Exam 2026 · Question 15
Ni methali gani inayoafikiana na kifungu ulichokisoma?
From Kiswahili — End of Year Assessment 2026 (Set 15) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali.
Siku moja Hassan alirudi nyumbani kwao mapema kuliko kawaida yake. Jambo hili lilifanyika kwa sababu alikuwa akihisi uchungu mwingi tumboni. Alipoenda hospitalini, daktari alimtibu na kumwambia aende nyumbani ajipumzishe ili maumivu yatulie. Alikuwa amekunywa maji yenye viini hatari.
Alipokaribia lango la kuingia kwao, alisikia sauti ikitoka kwenye zizi. Alitaka kujua yaliyokuwa yakijiri. Alipofika pale zizini, alipigwa na butwaa kwa yale aliyoyaona. Alikuta jirani yao Pwagu akimkama ng'ombe wao. Alipiga mayowe yaliyovutia majirani. Pwagu alikamatwa na kupelekwa kwenye ofisi ya chifu.
15. Ni methali gani inayoafikiana na kifungu ulichokisoma?
- APwagu hupata pwaguzi
- BSiku za mwizi ni arobaini
- CHasira hasara
- DMaji yakimwagika hayazoleki
Answer
B. Siku za mwizi ni arobaini
Pwagu aliiba mwishowe akakamatwa.