CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 2
Tofauti na mazoezi, Ndubi anapaswa kula nini?
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 14) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
Bango: Hujambo? Unaendeleaje?
Ndubi: Sijambo. Niko salama. Labda hali ya kwako.
Bango: Niko salama salmini. Kwani nini mbaya na wewe?
Ndubi: Sina mabaya ila nahisi kwamba sina nguvu.
Bango: Inaonekana kuwa hutilii maanani mambo ya afya yako. Je, unafanya mazoezi kila siku?
Ndubi: Unayoyasema ni kweli ndugu yangu. Huwa sifanyi mazoezi.
Bango: Unapaswa kujua kwamba mazoezi ya mwili huimarisha afya ya akili.
Ndubi: Ni kweli, ninakubaliana nawe. Nifanyeje?
Bango: Unachohitajika kufanya ni kuwa unapoamka asubuhi na jioni baada ya kuanza kazi unaweza kujiunga na sisi uwanjani tukimbie tukifanya zoezi. Zaidi ya hayo, usisahau kula chakula chenye afya.
Ndubi: Ninashukuru kwa mawaidha hayo uliyonipa. Tafadhali nipe muda niyatafakari.
2. Tofauti na mazoezi, Ndubi anapaswa kula nini?
- AMatunda pekee
- BNyama pekee
- CViazi pekee
- DLishe bora
Answer
D. Lishe bora
"Usisahau kula chakula chenye afya."
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Mazoezi husaidia vipi?Question 3
- Ifuatayo ni mifano ya mazoezi isipokuwaQuestion 4
- Mazungumzo haya yanahusu ?Question 5
- Kijijini kwa kina msimulizi ni wapi?Question 6
- Msimulizi alienda kusaidiana huko shambani. Walifanya haya yote ila nini?Question 7
- Babu alikuwa akifanya nini wakati msimulizi, ndugu zake na wazazi walipofika?Question 8