CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 8
Babu alikuwa akifanya nini wakati msimulizi, ndugu zake na wazazi walipofika?
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 14) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6-10.
Likizo iliyopita, tuliwatembelea babu na nyanya yetu huko Makueni. Ni wakulima hodari sana. Katika shamba lao, wamepanda mahindi, maharagwe, karoti na maua. Ungekuwa muda mzuri kwangu kwa sababu nilikuwa naongeza mwaka mmoja. Tulifika kijijini pamoja na wazazi na ndugu zangu wawili wakati wa jioni. Babu na nyanya walifurahi sana kutuona.
Babu yangu alikuwa amekaa chini ya mti mkubwa akila chakula chake. Walitukaribisha kwa furaha nyingi sana. Mara tukapewa chakula. Chakula chenyewe kilikuwa kitamu sana. Nyanya aliniahidi kuwa angenipa zawadi ya kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa siku iliyofuata. Kesho yake tulienda shambani kusaidia wafanyakazi wengine. Tulivuna karoti na maua mengine ambayo yaliuzwa tu hapo shambani. Tulifurahia sana.
8. Babu alikuwa akifanya nini wakati msimulizi, ndugu zake na wazazi walipofika?
- AAkilima
- BAkitazama runinga
- CAkila
- DAkiwa mkutanoni
Answer
C. Akila
Alikuwa akila chini ya mti.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Chakula cha adhuhuri huitwaje?Question 9
- Chakula walichopewa kilikuwa kitamu. Tunasema tamu kamaQuestion 10
- Barua hii iliandikwa muhula gani? Wa___Question 11
- Ni nani aliyemwandikia mwenzake wa kwanza?Question 12
- Tofauti na dini za Waafrika, ni nini kingine kilichukiza na wakoloni katika utamaduni wetu?Question 13
- Ni mifano mingapi iliyotolewa kuonesha kuwa tuna utamaduni mbalimbali nchini Kenya?Question 14