naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 7

Msimulizi alienda kusaidiana huko shambani. Walifanya haya yote ila nini?

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 14) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6-10.
Likizo iliyopita, tuliwatembelea babu na nyanya yetu huko Makueni. Ni wakulima hodari sana. Katika shamba lao, wamepanda mahindi, maharagwe, karoti na maua. Ungekuwa muda mzuri kwangu kwa sababu nilikuwa naongeza mwaka mmoja. Tulifika kijijini pamoja na wazazi na ndugu zangu wawili wakati wa jioni. Babu na nyanya walifurahi sana kutuona.
Babu yangu alikuwa amekaa chini ya mti mkubwa akila chakula chake. Walitukaribisha kwa furaha nyingi sana. Mara tukapewa chakula. Chakula chenyewe kilikuwa kitamu sana. Nyanya aliniahidi kuwa angenipa zawadi ya kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa siku iliyofuata. Kesho yake tulienda shambani kusaidia wafanyakazi wengine. Tulivuna karoti na maua mengine ambayo yaliuzwa tu hapo shambani. Tulifurahia sana.

7. Msimulizi alienda kusaidiana huko shambani. Walifanya haya yote ila nini?

  1. AKuuza maua
  2. BKutayarisha chajio
  3. CKuvuna karoti
  4. DKukata maua

Answer

B. Kutayarisha chajio

Hawakutayarisha chajio shambani.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test