naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 12

Ni nani aliyemwandikia mwenzake wa kwanza?

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 14) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma barua ifuatayo kisha ujibu maswali 11-12.
SHULE YA MSINGI YA NGURA,
S.L.P 48734,
KABUNDE.
12-6-2024.
Rafiki yangu, Hekima,
Pokea salamu nyingi kutoka kwangu. U hali gani? Mimi hapa ni mzima. Nina furaha nyingi kukueleza kwamba barua yako nimeipata leo hii.
Nimefurahishwa sana na yale uliyosema. Nimefurahi jinsi ulivyofanya katika mtihani wako wa mwanzo wa muhula huu. Baada ya hayo ningependa kukujulisha kwamba baba yangu amerudi kutoka ng’ambo. Aliniletea zawadi kemkem ambazo zinapendeza. Ukipata nafasi tafadhali nitembelee nikuzawadi na wewe pia. Ni hayo tu kwa sasa. Wasalimie ndugu zako.
Mimi wako,
Nasaha.

12. Ni nani aliyemwandikia mwenzake wa kwanza?

  1. AHekima
  2. BKabude
  3. CNasaha
  4. DHatujaambiwa

Answer

A. Hekima

Nasaha anasema "barua yako nimeipata", kwa hivyo Hekima ndiye aliyeandika kwanza.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test