naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 15

Kwa nini nchi ya Kenya haina utamaduni sawa?

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 14) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13-15.
Utamaduni ni jinsi binadamu anavyokabili maisha katika mazingira yake. Yote yanajumlisha ujuzi, imani, sanaa, maadili, sheria na desturi. Nchini Kenya hamna utamaduni wa kila mtu kwa sababu tuna makabila tofauti tofauti. Kwa mfano, kila jamii ina njia tofauti za kujenga nyumba zao. Tunasherehekea kuzaliwa kwa watoto kwa njia mbalimbali na hata kuwapa watoto majina.
Wakoloni walipokuja nchini, hawakupenda tamaduni na dini zetu. Kulingana na wao, Waafrika hawakumwamini Mwenyezi Mungu. Hawakupenda vyakula vyetu, dawa zetu na hata mfumo wa elimu yetu. Hii ilifanya Waafrika kuacha utamaduni wao na kuanza kuiga ya wakoloni.

15. Kwa nini nchi ya Kenya haina utamaduni sawa?

  1. AWakenya wako wengi
  2. BKenya ina watu wachache
  3. CKila jamii inafanya vitu kwa njia mbalimbali.
  4. DWakenya bado hawajaamua

Answer

C. Kila jamii inafanya vitu kwa njia mbalimbali.

Kila jamii ina njia zake.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test