naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 4

Ifuatayo ni mifano ya mazoezi isipokuwa

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 14) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
Bango: Hujambo? Unaendeleaje?
Ndubi: Sijambo. Niko salama. Labda hali ya kwako.
Bango: Niko salama salmini. Kwani nini mbaya na wewe?
Ndubi: Sina mabaya ila nahisi kwamba sina nguvu.
Bango: Inaonekana kuwa hutilii maanani mambo ya afya yako. Je, unafanya mazoezi kila siku?
Ndubi: Unayoyasema ni kweli ndugu yangu. Huwa sifanyi mazoezi.
Bango: Unapaswa kujua kwamba mazoezi ya mwili huimarisha afya ya akili.
Ndubi: Ni kweli, ninakubaliana nawe. Nifanyeje?
Bango: Unachohitajika kufanya ni kuwa unapoamka asubuhi na jioni baada ya kuanza kazi unaweza kujiunga na sisi uwanjani tukimbie tukifanya zoezi. Zaidi ya hayo, usisahau kula chakula chenye afya.
Ndubi: Ninashukuru kwa mawaidha hayo uliyonipa. Tafadhali nipe muda niyatafakari.

4. Ifuatayo ni mifano ya mazoezi isipokuwa

  1. Akulala
  2. Bmbio
  3. Cmchezo wa kandanda
  4. Dkuruka kamba

Answer

A. kulala

Kulala si zoezi.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test