CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 15
Tumeambiwa kuwa mti mkubwa ulioko Kalifonia
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 13 hadi 15.
Miti huvutia macho. Watu wengi hupenda nyumba zao zikizungukwa na miti. Hoteli nyingi kubwa zimejengwa katika maeneo yenye miti mingi. Ukiangalia mti, kwanza, unaona shina ambalo hushikilia sehemu za juu kama matawi, majani, maua na matunda. Kwa chini, shina huonekana kuzeeka na lenye mikwaruzo. Juu, shina huonekana changa na laini.
Mti mrefu zaidi leo ni zaidi ya futi mia tatu na sitini kwa urefu. Mti huu unapatikana Kalifonia, huko Marekeni. Mti huu huweza kutoa mbao za kujengea zaidi ya nyumba mia tatu. Chini kuna mizizi iliyojipenyeza mchangani na kusambaa.
Kila mmoja wetu, wakubwa kwa wadogo, anastahili kuifanya dunia maridadi kwa kupanda miti.
15. Tumeambiwa kuwa mti mkubwa ulioko Kalifonia
- Ani mzuri kwa kufanywa kuni.
- Bunaweza kutumia kujengea nyumba nyingi.
- Cuna shina laini.
- Duna mizizi inayojipenyeza hewani.
Answer
B. unaweza kutumia kujengea nyumba nyingi.
Mbao za nyumba mia tatu.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Gani ni laki moja na moja?Question 21
- Nini wingi wa sentensi hii: Nyani amekula nyanya.Question 22
- Jibu maamkuzi yafuatayo: Chewa?Question 23
- Jaza nafasi iliyoachwa wazi kwa jibu mwafaka. Msimu uliopita, tulivamiwa na viwavi ___ waliharibu mimea yote.Question 24
- Chagua sentensi sawa kisarufiQuestion 25
- Ni neno lipi kati ya haya halipatikani katika ngeli ya Li-li.Question 26