naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 2

Ni faida ipi ya kufanya kazi za nyumbani kabla ya shule?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Mazungumzo

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1 – 5.
Neema: Habari za asubuhi, Mariam?
Mariam: Nzuri sana, asubuhi njema kwako pia Neema.
Neema: Umejiandaa kwenda shuleni leo?
Mariam: Ndiyo. Niliamka mapema nikapanga kitanda, nikafagia sebule na nikamsaidia mama kupika uji. Wewe umefanya nini?
Neema: Mimi nimeosha vyombo, nikampeleka mdogo wangu kwa jirani halafu nikafagia uwanja.
Mariam: Ni vizuri sana kufanya kazi za nyumbani kabla ya shule. Inatufundisha uwajibikaji.
Neema: Ni kweli. Hata mwalimu wetu alisema wanafunzi wanaosaidia nyumbani huwa na nidhamu na heshima shuleni.
Mariam: Nimeskia pia leo tutakuwa na somo la Kiswahili kwanza. Je, umefanya kazi ya nyumbani?
Neema: Ndiyo, nilijaribu kujibu maswali ya kuhusu sentensi na alama za uandishi wewe je?
Mariam: Niliandika sentensi tano na nikatumia alama sahihi.
Neema: Utajifunza zaidi darasani. Baada ya masomo, tutacheza michezo.
Mariam: Bila shaka! Mimi napendelea kuruka kamba, lakini pia nataka kucheza mpira wa miguu.
Neema: Hata mimi napenda michezo lakini tusisahau kurudia masomo jioni. Siyo?
Mariam: Ni kweli. Mchezo ni burudani, lakini masomo ndiyo yatakayotufanikisha maishani.
Neema: Haya maneno yamenifurahisha. Hebu tuende sasa kabla kengele ya kuingia ipigwe.
Mariam: Twende kwa haraka basi.

2. Ni faida ipi ya kufanya kazi za nyumbani kabla ya shule?

  1. AInawafundisha uwajibikaji wa nidhamu
  2. BInawapa muda wa kucheza
  3. CInawapotezea muda
  4. DInawafanya wachoke darasani

Answer

A. Inawafundisha uwajibikaji wa nidhamu

"Inatufundisha uwajibikaji."

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test