CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 1
Ni somo lipi lililotajwa kuwa la kwanza na kwa nini wasichana walifanya kazi ya nyumbani mapema?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1 – 5.
Neema: Habari za asubuhi, Mariam?
Mariam: Nzuri sana, asubuhi njema kwako pia Neema.
Neema: Umejiandaa kwenda shuleni leo?
Mariam: Ndiyo. Niliamka mapema nikapanga kitanda, nikafagia sebule na nikamsaidia mama kupika uji. Wewe umefanya nini?
Neema: Mimi nimeosha vyombo, nikampeleka mdogo wangu kwa jirani halafu nikafagia uwanja.
Mariam: Ni vizuri sana kufanya kazi za nyumbani kabla ya shule. Inatufundisha uwajibikaji.
Neema: Ni kweli. Hata mwalimu wetu alisema wanafunzi wanaosaidia nyumbani huwa na nidhamu na heshima shuleni.
Mariam: Nimeskia pia leo tutakuwa na somo la Kiswahili kwanza. Je, umefanya kazi ya nyumbani?
Neema: Ndiyo, nilijaribu kujibu maswali ya kuhusu sentensi na alama za uandishi wewe je?
Mariam: Niliandika sentensi tano na nikatumia alama sahihi.
Neema: Utajifunza zaidi darasani. Baada ya masomo, tutacheza michezo.
Mariam: Bila shaka! Mimi napendelea kuruka kamba, lakini pia nataka kucheza mpira wa miguu.
Neema: Hata mimi napenda michezo lakini tusisahau kurudia masomo jioni. Siyo?
Mariam: Ni kweli. Mchezo ni burudani, lakini masomo ndiyo yatakayotufanikisha maishani.
Neema: Haya maneno yamenifurahisha. Hebu tuende sasa kabla kengele ya kuingia ipigwe.
Mariam: Twende kwa haraka basi.
1. Ni somo lipi lililotajwa kuwa la kwanza na kwa nini wasichana walifanya kazi ya nyumbani mapema?
- AKiingereza, kwa sababu hawana shughuli nyingi
- BKiswahili, kwa sababu wanapenda kuwa tayari
- CSayansi, kwa sababu wanapenda michezo
- DHisabati, kwa sababu walitaka kucheleza muda
Answer
B. Kiswahili, kwa sababu wanapenda kuwa tayari
Somo la Kiswahili kwanza.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Ni faida ipi ya kufanya kazi za nyumbani kabla ya shule?Question 2
- Wasichana wanasema nini kuhusu michezo na masomo?Question 3
- Mwalimu wao aliwafundisha nini?Question 4
- Mazungumzo haya yanafundisha wanafunzi mambo gani mawili muhimu?Question 5
- Kulingana na ufahamu huu wahenga ni nani?Question 6
- Kamilisha methali: HeshimaQuestion 7