CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 4
Mwalimu wao aliwafundisha nini?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1 – 5.
Neema: Habari za asubuhi, Mariam?
Mariam: Nzuri sana, asubuhi njema kwako pia Neema.
Neema: Umejiandaa kwenda shuleni leo?
Mariam: Ndiyo. Niliamka mapema nikapanga kitanda, nikafagia sebule na nikamsaidia mama kupika uji. Wewe umefanya nini?
Neema: Mimi nimeosha vyombo, nikampeleka mdogo wangu kwa jirani halafu nikafagia uwanja.
Mariam: Ni vizuri sana kufanya kazi za nyumbani kabla ya shule. Inatufundisha uwajibikaji.
Neema: Ni kweli. Hata mwalimu wetu alisema wanafunzi wanaosaidia nyumbani huwa na nidhamu na heshima shuleni.
Mariam: Nimeskia pia leo tutakuwa na somo la Kiswahili kwanza. Je, umefanya kazi ya nyumbani?
Neema: Ndiyo, nilijaribu kujibu maswali ya kuhusu sentensi na alama za uandishi wewe je?
Mariam: Niliandika sentensi tano na nikatumia alama sahihi.
Neema: Utajifunza zaidi darasani. Baada ya masomo, tutacheza michezo.
Mariam: Bila shaka! Mimi napendelea kuruka kamba, lakini pia nataka kucheza mpira wa miguu.
Neema: Hata mimi napenda michezo lakini tusisahau kurudia masomo jioni. Siyo?
Mariam: Ni kweli. Mchezo ni burudani, lakini masomo ndiyo yatakayotufanikisha maishani.
Neema: Haya maneno yamenifurahisha. Hebu tuende sasa kabla kengele ya kuingia ipigwe.
Mariam: Twende kwa haraka basi.
4. Mwalimu wao aliwafundisha nini?
- AMichezo
- BKuosha vyombo
- CMichezo ya kukimbia
- DNidhamu na heshima
Answer
D. Nidhamu na heshima
Wanaosaidia nyumbani huwa na nidhamu na heshima.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Mazungumzo haya yanafundisha wanafunzi mambo gani mawili muhimu?Question 5
- Kulingana na ufahamu huu wahenga ni nani?Question 6
- Kamilisha methali: HeshimaQuestion 7
- Watoto wanastahili kuwaheshimu watu hawa wote isipokuwaQuestion 8
- Kamilisha nafasi iliyowekwa herufi HQuestion 9
- Barua hii ni ya aina gani?Question 10