naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 6

Kulingana na aya ya kwanza ni kweli

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6 hadi la 9.
Shule zinapofungwa wazazi wangu hunipeleka kuwatembelea babu na nyanya. Babu hunifunza jinsi ya kulima shambani. Yeye huniekeleza jinsi ya kuinua jembe na kupalilia mimea. Mara nyingi huwa napalilia mboga na mihindi. Mboga anazozipenda ni kama mchicha, sukumawiki na mkunde.
Mkunde hutupa kunde na mbegu zake hutumika kama nafaka. Nafaka hizi zaweza sagwa na kuwa unga wa uji au kama kitoweo. Unaweza kuuza kunde na nafaka hizi sokoni ili upate hela za matumizi mengi.
Mchicha ndio mboga tamu ya bibi. Yeye huchanganya mchicha kwa kila chakula. Si wali, si pure si sima. Bibi husema kuwa mboga hizi zina madini ambayo huwezesha afya kuwa bora.
Baada ya likizo babu hunipa zawadi. Zawadi hizi ni kama kuku, sungura na njiwa. Tangu nianze kuwatembelea babu na nyanya nimeweza kuzawadiwa sungura wanne. Sungura wawili ni weupe na wengine ni weusi. Sungura wangu wakiwa wakubwa nitachinja mmoja mweupe awe kitoweo na wa kijivu nimpe mwalimu wangu wa Kiswahili kama zawadi.

6. Kulingana na aya ya kwanza ni kweli

  1. Amsimulizi hujipeleka kwa nyanya
  2. Bmsimulizi hutembelea bibi yake
  3. Cbabu wa msimulizi hapendi kilimo
  4. Dnyanyaye msimulizi hapendi mboga

Answer

B. msimulizi hutembelea bibi yake

Wazazi humpeleka kuwatembelea babu na nyanya.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test