CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 5
Chagua maagano ambayo Pato alitumia.
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Maagano
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 1 hadi la 5.
(Ni barabarani, Pato anakutana na Kaka akiwa amebeba rato.)
Pato: Hujambo Kaka?
Kaka: Sijambo Pato. Umeadimika sana kama wali wa daku. (wakitabasamu.)
Pato: Si sana. Je, unatoka wapi na rato? Unaonekana kuwa umechoka sana kama punda wa dobi.
Kaka: Mimi pamoja na marafiki wenzangu tumekuwa tukifanya bidii shambani.
Pato: Hewaa! Jambo zuri sana. Nami nimetoka uwanjani kufanya mazoezi. Tangu mwezi uliopita nimekuwa nikifanya mazoezi. Ningetaka kuwa mchezaji bora. Mwezi ujao nitaelekea Marekani. Nimealikwa na timu moja kufanya majaribio. Sina budi kumshukuru Mungu kwa ufanisi huo. Lazima nijikaze kisabuni ili nifaulu.
Kaka: Hongera. Uamuzi huo ni wa busara mwenzangu. Ningependa nifike nyumbani ili nioge na nipumzike kiasi.
Pato: __5__ Kaka.
Kaka: Buriani dawa. (Wakisalimiana na kuondoka)
5. Chagua maagano ambayo Pato alitumia.
- ABuriani
- BKwaheri
- CAlamsiki
- DTuonane
Answer
A. Buriani
Jibu la "Buriani" ni "Buriani dawa".
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Kulingana na aya ya kwanza ni kweliQuestion 6
- Andika zao moja ambalo hupandwa na babu wa msimulizi.Question 7
- Bibi wa msimulizi hupenda mchicha kwa kuwa ___Question 8
- Msimulizi ana sungura wangapi weusi?Question 9
- Ni chakula kipi huandaliwa kwa kuchanganya mahindi na maharagwe?Question 10
- Kati ya vyakula vilivyotajwa, ni kipi huwa kinywaji?Question 11