naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 8

Bibi wa msimulizi hupenda mchicha kwa kuwa ___

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6 hadi la 9.
Shule zinapofungwa wazazi wangu hunipeleka kuwatembelea babu na nyanya. Babu hunifunza jinsi ya kulima shambani. Yeye huniekeleza jinsi ya kuinua jembe na kupalilia mimea. Mara nyingi huwa napalilia mboga na mihindi. Mboga anazozipenda ni kama mchicha, sukumawiki na mkunde.
Mkunde hutupa kunde na mbegu zake hutumika kama nafaka. Nafaka hizi zaweza sagwa na kuwa unga wa uji au kama kitoweo. Unaweza kuuza kunde na nafaka hizi sokoni ili upate hela za matumizi mengi.
Mchicha ndio mboga tamu ya bibi. Yeye huchanganya mchicha kwa kila chakula. Si wali, si pure si sima. Bibi husema kuwa mboga hizi zina madini ambayo huwezesha afya kuwa bora.
Baada ya likizo babu hunipa zawadi. Zawadi hizi ni kama kuku, sungura na njiwa. Tangu nianze kuwatembelea babu na nyanya nimeweza kuzawadiwa sungura wanne. Sungura wawili ni weupe na wengine ni weusi. Sungura wangu wakiwa wakubwa nitachinja mmoja mweupe awe kitoweo na wa kijivu nimpe mwalimu wangu wa Kiswahili kama zawadi.

8. Bibi wa msimulizi hupenda mchicha kwa kuwa ______

Answer

una madini ambayo huwezesha afya kuwa bora

"mboga hizi zina madini".

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test