CBC Grade 4 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 2
Afya mbaya huletwa na ___
From Kiswahili — KPSEA Midterm Assessment 2025 Set 2 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 1 - 5.
Mazingira yetu lazima yawe safi. Tunafaa kupanda miti mingi. Miti huleta hewa safi na mvua. Tunapata matunda kutokana na miti. Tusiharibu maji ya mito na mifereji. Mazingira machafu huleta afya mbaya. Nzi na mbu huleta magonjwa. Mbu huleta ugonjwa wa malaria na nzi huleta ugonjwa wa kipindupindu.
Tuweke mazingira yetu safi ili tusipate magonjwa. Tunaweza kuweka mazingira yetu safi kwa njia mbalimbali. Tumia choo unapoenda haja. Tupa taka kwenye pipa kisha uzichome. Tusichafue mito kwa uchafu, tufagie tunapoishi na mwisho tusikate miti ovyo.
2. Afya mbaya huletwa na _____________
- Amvua
- Bnzi
- Cmbu
- Dmazingira machafu.
Answer
D. mazingira machafu.
Kifungu kinasema, "Mazingira machafu huleta afya mbaya." Nzi na mbu huleta magonjwa yanayotokana na uchafu huo.