CBC Grade 4 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 5
Kitate cha neno taka ni ___
From Kiswahili — KPSEA Midterm Assessment 2025 Set 2 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 1 - 5.
Mazingira yetu lazima yawe safi. Tunafaa kupanda miti mingi. Miti huleta hewa safi na mvua. Tunapata matunda kutokana na miti. Tusiharibu maji ya mito na mifereji. Mazingira machafu huleta afya mbaya. Nzi na mbu huleta magonjwa. Mbu huleta ugonjwa wa malaria na nzi huleta ugonjwa wa kipindupindu.
Tuweke mazingira yetu safi ili tusipate magonjwa. Tunaweza kuweka mazingira yetu safi kwa njia mbalimbali. Tumia choo unapoenda haja. Tupa taka kwenye pipa kisha uzichome. Tusichafue mito kwa uchafu, tufagie tunapoishi na mwisho tusikate miti ovyo.
5. Kitate cha neno taka ni _________
- Adada
- Btakataka
- Cdaka
- Dsitaki.
Answer
C. daka
Vitate ni maneno yanayokaribiana kimatamshi lakini yanatofautiana kwa sauti moja. Taka na daka zinatofautiana kwa sauti /t/ na /d/ pekee.