naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 5

Kulingana na kifungu, polisi wakifumbia macho visa vya utovu wa usalama

From Test 121 — Kiswahili Mukula wa 1 2025 · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Soma kifungu hiki kisha ujibu.
Usalama wa nchi yoyote hutegemea mambo mbalimbali. Kwanza ni jinsi ambavyo asasi za kiusalama zinavyowajibika katika kushughulikia suala hilo. Asasi zenyewe zikilegea, usalama hudorora. Mathalani, katika nchi ambamo askari hupokea hongo na kuyafumbia macho matendo ya uhalifu, wananchi hutaabika sana kutokana na visa vya utovu wa usalama.

Mchango wa wananchi wenyewe hauwezi kupuuzwa. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo. Wananchi hawafai kupakata mikono ili serikali iwalindie usalama wao. Kila mmoja hana budi kukaa ange ili kuwatambua watu wenye nia ya kuvuruga usalama katika jamii. Vitendo vya aina hiyo vinafaa kuzuiliwa kabla havijatokea kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba.

Kulingana na kifungu, polisi wakifumbia macho visa vya utovu wa usalama

  1. AWananchi huchukua sheria mkononi
  2. BVisa vya uhalifu huongezeka
  3. CWatu hulaumu serikali
  4. DMatukio ya utovu wa usalama hupungua

Answer

B. Visa vya uhalifu huongezeka

Jibu sahihi ni: Visa vya uhalifu huongezeka.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test