naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 4

Umejifunza nini kutokana na hadithi hii?

From Test 121 — Kiswahili Mukula wa 1 2025 · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Soma/Read the source text, then answer.
Maria alikuwa msichana mwerevu. Alisomea katika shule ya Elimubora. Walimu na wanafunzi walimpenda kutokana na werevu na ukarimu wake. Kila siku marafiki hao walimganda kama kupe.

Jambo la ajabu ni kuwa hakuna mtu aliyewajua wazazi wa Maria. Kila mara kulipokuwa na mkutano wa wazazi, Maria alitoa visingizio vya kila aina. Mara alisema kuwa mama yake alikuwa mgonjwa au ameenda safarini. Hakutaka rafiki yeyote amtembelee kwao.

Siku moja rafiki yake anayeitwa Shamila alimfuata kisirisiri hadi kwao. Mama yake alisikia mlango ukibishwa akafungua. Hapo ndipo Shamila alipoelewa ni kwa nini Maria hakutaka mama yake aonekane. Alikuwa na alama nyingi usoni zilizoachwa na majeraha ya moto.

Mama aliandaa chai akawamiminia Shamila na Maria. Alianza kuwasimulia kisa cha miaka kadhaa iliyopita. Aliwaeleza kuhusu mama mmoja ambaye aliingia katika nyumba iliyokuwa ikichomeka ili amwokoe binti yake. Alifaulu kumtolea mtoto huyo dirishani lakini yeye hakuwa na bahati. Alichomeka vibaya alipokuwa akitoka kwani hakuwa na budi kupitia kwenye moto.

“Mtoto huyo ana bahati sana. Mama yake alijitoa mhanga ili amwokoe. Ama kweli uchungu wa mwana aujuaye ni mama,” Shamila alisema kwa masikitiko.

Mama Maria aliingia chumbani akatoka na picha ya msichana mrembo kama hurulaini. “Je, mnatambua aliye pichani?” aliwauliza mabinti wale. Maria alitazama picha ile kwa makini. Mara moja alitambua kidani ambacho mama yake alipenda kuvaa. Ghafla akajua yaliyojiri. Kumbe mama yake alipoteza uzuri wake akimwokoa.

“Nisamehe mama,” alilia huku akimkumbatia mamaye. Tangu siku hiyo, alimwona mama yake kama shujaa wake. Aliandamana naye kila mahali. Aligundua kuwa urembo wa kweli haumo kwenye sura bali matendo yetu.

Umejifunza nini kutokana na hadithi hii?

Answer

Urembo wa kweli umo katika matendo mema na tunapaswa kuthamini kujitolea kwa wazazi.

A complete answer could be: Urembo wa kweli umo katika matendo mema na tunapaswa kuthamini kujitolea kwa wazazi.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test