CBC Grade 9 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 9
Eleza ujumbe wa aya ya kwanza kwa sentensi moja.
From Test 121 — Kiswahili Mukula wa 1 2025 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufupisho na Kusoma kwa Mapana
Soma/Read the source text, then answer.
Lugha ya taifa ni muhimu sana. Katika nchi yoyote ile, huwepo watu wenye asili mbalimbali. Tofauti zao hujitokeza waziwazi kupitia lugha mbalimbali wanazoongea. Ni jukumu la lugha ya taifa kuwaunganisha watu hao ili waweze kuelewana na kushirikiana ipasavyo.
Hebu fikiria hali ingekuwa vipi ikiwa kila mmoja nchini angezungumza lugha yake binafsi. Je, watu wangeweza kufanya kazi pamoja? Nchi ingeweza kuendelea? Ukijiuliza maswali haya ndipo itakapobainika kwako kuwa maendeleo ya taifa lolote hutegemea uwepo wa lugha unganishi ambayo ni lugha ya taifa. Hii ndiyo sababu kila taifa huhakikisha kuwa lugha yake ya taifa ni somo la lazima katika nchi hiyo.
Nchini Kenya, Kiswahili ni lugha ya taifa. Lugha hii imechangia kuunganisha zaidi ya makundi arubaini na mawili ya kikabila ambayo hupatikana humu nchini. Hali kadhalika, Kiswahili ni mojawapo ya lugha rasmi nchini. Mtu hafai kuona aibu anapotumia lugha hii katika shughuli yoyote ile, iwe shuleni, sokoni, ofisini au hata bungeni.

Answer
Lugha ya taifa huunganisha watu wa asili na lugha mbalimbali ili waelewane na kushirikiana.
A complete answer could be: Lugha ya taifa huunganisha watu wa asili na lugha mbalimbali ili waelewane na kushirikiana.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- Fupisha ujumbe ulioangaziwa katika aya ya pili kwa maneno yasiyozidi 9.Question 10
- Andika habari kuu iliyo katika aya ya tatu kwa sentensi moja.Question 11
- Andika kichwa kifaacho kwa kifungu hiki.Question 12
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza pengo 13.Question 13
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza pengo 14.Question 14
- Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza pengo 15.Question 15