naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 11

Andika habari kuu iliyo katika aya ya tatu kwa sentensi moja.

From Test 121 — Kiswahili Mukula wa 1 2025 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufupisho na Kusoma kwa Mapana

Soma/Read the source text, then answer.
Lugha ya taifa ni muhimu sana. Katika nchi yoyote ile, huwepo watu wenye asili mbalimbali. Tofauti zao hujitokeza waziwazi kupitia lugha mbalimbali wanazoongea. Ni jukumu la lugha ya taifa kuwaunganisha watu hao ili waweze kuelewana na kushirikiana ipasavyo.

Hebu fikiria hali ingekuwa vipi ikiwa kila mmoja nchini angezungumza lugha yake binafsi. Je, watu wangeweza kufanya kazi pamoja? Nchi ingeweza kuendelea? Ukijiuliza maswali haya ndipo itakapobainika kwako kuwa maendeleo ya taifa lolote hutegemea uwepo wa lugha unganishi ambayo ni lugha ya taifa. Hii ndiyo sababu kila taifa huhakikisha kuwa lugha yake ya taifa ni somo la lazima katika nchi hiyo.

Nchini Kenya, Kiswahili ni lugha ya taifa. Lugha hii imechangia kuunganisha zaidi ya makundi arubaini na mawili ya kikabila ambayo hupatikana humu nchini. Hali kadhalika, Kiswahili ni mojawapo ya lugha rasmi nchini. Mtu hafai kuona aibu anapotumia lugha hii katika shughuli yoyote ile, iwe shuleni, sokoni, ofisini au hata bungeni.

Andika habari kuu iliyo katika aya ya tatu kwa sentensi moja.

Answer

Kiswahili ni lugha ya taifa na rasmi inayowaunganisha Wakenya.

A complete answer could be: Kiswahili ni lugha ya taifa na rasmi inayowaunganisha Wakenya.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test