naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 7

Methali ‘kinga ni bora kuliko tiba’ imetumika kwa maana gani katika kifungu?

From Test 121 — Kiswahili Mukula wa 1 2025 · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Soma/Read the source text, then answer.
Usalama wa nchi yoyote hutegemea mambo mbalimbali. Kwanza ni jinsi ambavyo asasi za kiusalama zinavyowajibika katika kushughulikia suala hilo. Asasi zenyewe zikilegea, usalama hudorora. Mathalani, katika nchi ambamo askari hupokea hongo na kuyafumbia macho matendo ya uhalifu, wananchi hutaabika sana kutokana na visa vya utovu wa usalama.

Mchango wa wananchi wenyewe hauwezi kupuuzwa. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo. Wananchi hawafai kupakata mikono ili serikali iwalindie usalama wao. Kila mmoja hana budi kukaa ange ili kuwatambua watu wenye nia ya kuvuruga usalama katika jamii. Vitendo vya aina hiyo vinafaa kuzuiliwa kabla havijatokea kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba.

Methali ‘kinga ni bora kuliko tiba’ imetumika kwa maana gani katika kifungu?

Answer

Ni afadhali kuzuia uhalifu au tishio la usalama kabla halijatokea kuliko kushughulikia madhara yake baadaye.

A complete answer could be: Ni afadhali kuzuia uhalifu au tishio la usalama kabla halijatokea kuliko kushughulikia madhara yake baadaye.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test